Spika wa Bunge Marekani, akataa mwaliko wa Zelensky

SPIKA wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy amekataa mwaliko wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy wa kuzuru taifa hilo, CNN imeripoti.

Licha ya changamoto za kivita wanazokutana nazo Ukraine kutoka kwa Mrusi, ambazo kimsingi McCarthy alitakiwa kwenda kuziona, kiongozi huyo amesema hana haja ya kwenda na badala yake apewe taarifa kwa njia zingine.

Msimamo wa spika huyo ni kwamba anaiunga mkono Ukraine katika vita dhidi ya Urusi ila Warepublican waliochukua madaraka ya bunge hilo mwezi Januari, hawatatoa nafasi kuisaidia Ukraine.

Marekani imeipa Ukraine dola bilioni 32 tangu Urusi ianze uvamizi wake Februari 24,2023 ila baadhi ya viongozi wa Republican wenye siasa kali wamekataa kuitumia Ukraine msaada zaidi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button