Stara: Sitaacha kuimba nyimbo za zamani
DAR ES SALAAM; Msanii wa Bongo fleva, Stara Thomas amesema licha ya kuokoka, lakini ataendelea kuimba nyimbo zake za zamani kwa kuwa Roho Mtakatifu anamuongoza kuimba muziki huo.
“Nimeokoka pia ni Mchungaji, lakini sijaachana na kuimba muziki wangu wa zamani ambao watu wanasema ni miziki ya kidunia, ndio tunaimba kwa sababu tupo duniani lazima tuimbe.
“Kwa kuwa hatuimbi matusi wala kinyume na maadili, ila ni kuburudisha na kuelimisha, badala yake Roho Mtakatifu ndiyo ananiongoza jinsi ya kuimba bongo fleva kwa usahihi zaidi ninapokuwa jukwaani,”amesema Stara
Amesema Stara ni tofauti na wasanii wengine waliookoka na kuacha kabisa kuimba muziki wa kidunia na kuhamia kwenye muziki wa kiroho pekee.