Stars yatanguliza mguu moja fainali AFCON

TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za michuano ya Mataifa ya Afika (Afcon), baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo.

Matokeo hayo yameifanya Stars ifikishe pointi 7 nyuma ya vinara Algeria ambao tayari wameshafuzu fainali hizo, ambapo muda huu wanacheza na Uganda, yenye pointi nne, mchezo unaofanyika nchini Uganda. Bao la Stars lilifungwa na Simon Msuva.

Mchezo wa mwisho Taifa Stars itamaliza ugenini dhidi ya Algeria, wakati Uganda itakuwa ugenini dhidi ya Niger.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *