Stendi ya Makumbusho haitahamishwa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Albert Chalamila amesema stendi ya Makumbusho haitahama kwenda stendi mpya ya Mwenge badala yake utawekwa utaratibu maalum ili stendi zote zitumike kikamifu.

Kauli hiyo ya Chalamika ilikuja mara baada ya mfanyabishara Samora Wiliam maarufu kama Big kuuliza hatima ya wafanyabishara wa soko la Makubusho baada ya stendi hiyo kuhamia Mwenge.

“Soko la Makumbusho ni bega kwa bega na stendi ya Makumbusho na tunasikia za chini chini kuwa stendi hii ya Makumbusho inahama baada ya stendi ya Mwenge kukamilika sasa hizi biashara tunategemea magari zitakapohama biashara zitayumba tunaomba hilo liangaliwe,”ameeleza Big.

Akijibu hoja hiyo Chalamila amesema hakuna mpango wowote wa kuondoa magari katika stendi ya Makumbusho na kusisitiza kuwa magari yatakuwa yakiingia na kutoka katika stendi zote.

“Stendi ya makumbusho haihami hili bado linaendelea kama kawaida hakuna kitu ambacho kitabadilika magari yataingia na kutoka kama kawaida,”amesema.

Aidha, Chalamila amewatoa hofu kwa kusema kuwa wataweka utaratibu maalum wa magari kuingia na kutoka  katika stendi zote ikiwemo yale yenye ruti ndefu.

“Kuna magari hapa yanaingia lakini yanatoka mbali hiyo hapa yataingia na kupita na wateja mtapata tu msiwe na wasiwasi.

Habari Zifananazo

Back to top button