Steve Nyerere: Wanasiasa tumieni majukwaa vizuri

DAR ES SALAAM: Msanii wa Filamu nchini na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amewataka wanasiasa kuacha kutoa kauli mbaya ‘matusi’ mitandaoni, na majukwaani wanapozungumza na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve Nyerere’ amedai kuwa wanasiasa mbalimbali wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na kutumia lugha zisizofaa.

“Nawaomba wanasiasa kufanya siasa safi bila kutumia matusi pindi wanapo kuwa kwenye majukwaa mbalimbali pamoja na kwenye mitandao ya kijamii wananchi wanataka kusikia hoja sio lugha chafu.”

“Nimesikitishwa na kitendo cha kijana mmoja kutoka Mbeya ambaye ‘jina kapuni’ ambaye hutumia mitandao ya kijamii kuwatukana viongozi wa siasa kitu ambacho ni kinyume na uzalendo na sio siasa yetu.

Hata hivyo amewaomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwatafuta na kuwashughulikia wote wanaotumia mitandao kwa kuwatukana viongozi kwani mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika katika maendeleo na sio kauli chafu.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button