DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amewaomba watanzania kuwachangia huduma za vitu mbali mbali waathirika wa mafuriko Hanang.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Programu ya Mama amstiri Mwanamke jijini Dar es Salaam Steve Nyerere amesema kuwa taasisi hiyo imelenga kutoa taulo kwa Wanawake 200,00 sambamba na kutoa miswaki na nguo za ndani.
“Tumekuwa tukichangia harusi na kutoa zawadi na kufanya Birthday lakini tumelisahau kundi la watu waliopata matatizo.”amesema Steve Nyerere.
Steve Nyerere amesema unavyoweza kusherekea sikukuu unahitaji kujua kuna jamii kundi la wanawake wapo Hanang wanahitaji furaha kutoka kwako kupewa kipaumbele katika kulisaidia kundi hilo.