‘Suala la elimu tasnia ya habari litapatiwa ufumbuzi’

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema suala la elimu katika tasnia ya habari, linatafutiwa mwarobaini.

Amesema, wanapendekeza waandishi waliopo kwenye tasnia ya habari ambao hawana vigezo, wasiondolewe na badala yake wapate mafunzo wakiwa kazini, huku wanaoingia lazima wakidhi vigezo vya elimu iliyowekwa.

“Tungependa waandishi waliopo kazini wasiondolewe, bali wapate mafunzo wakiwa kazini, lakini wale wapya wanaotaka kuingia katika tasnia ya habari, lazima wakidhi vigezo vya kuwa na elimu walau diploma,” amesema Balile.

Amesema sio kila anayeweza kusoma na kuandika anaweza kuwa mwandishi,  bali uandishi ni taaluma iliyo na misingi yake.

“Kuna kipaji na taaluma, ukiwa na kipaji basi lazima upate misingi ya taaluma hapo unakuwa mwandishi mzuri, kila taaluma ina misingi yake,”  amaesema Balile.

Habari Zifananazo

Back to top button