Suala la Panya Road latua bungeni

#HABARI: Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, ameiagiza serikali kuchukua hatua za haraka kushughulikia vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na vikundi vya kihalifu kama Panya Road.-

Spika Dk Tulia ametoa maagizo hayo leo Septemba 15, wakati wa kikao cha Bunge kufuatia hoja ya dharura iliyowasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum, Bahati Ndigo aliyeomba shughuli za bunge ziahirishwe kwa muda kujadili kuhusu usalama wa raia na kuongezeka kwa vitendo hivyo vinavyoathiri maisha ya watu.

#HabarileoUPDATES

Habari Zifananazo

Back to top button