Suarez afungua akaunti ya mabao Miami
LUIS Suarez amefunga mabao yake ya kwanza akiwa na Inter Miami wakati Lionel Messi akiweka kambani mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi Orlando City ligi ya MLS.
Suarez, ambaye alishindwa kufunga katika mechi zake mbili za kwanza za MLS, alifunga mabao mawili katika dakika ya 4 na 11.
Suarez bila ubinafsi alimtengenezea Rob Taylor kabla ya Messi kufunga bao la kichwa akiunganisha krosi ya Suarez.
Mshambulizi huyo wa zamani wa Liverpool na Barcelona alijiunga na Miami mwezi Desemba baada ya kucheza na Nacional ya Uruguay na Gremio ya Brazil.