Suarez kumfuata Messi

UMESIKIA huko? Uswahiba wa Lionel Messi na Luis Suarez unaendelea kudhihirika baada ya taarifa kuwa Suarez anafikiria kuvunja mkataba na Gremio na kumfuata Messi Miami.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Suarez na Gremio wamekubaliana katika hatua hiyo licha ya kwamba mkataba wa mchezaji huyo ulibaki mwaka mmoja.

Suarez alijiunga na Gremio akitokea Nacional ya Uruguay, ambako alienda baada ya kuitumikia Atletico Madrid.

Advertisement

Suarez sasa ataunga na Messi katika klabu hiyo iliyopo nchini Marekani.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *