Sudan Kusini yaunga mkono amani DRC

SERIKALI ya Sudan Kusini imeunga mkono mpango wa amani wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambayo imeahidi kutoa wanajeshi 750 kwa ajili ya kulinda amani DRC.

Imesema baada ya muda mrefu wa malumbano na migogoro iliyogharimu maisha ya maelfu ya wananchi katika eneo la Mashariki mwa DRC, hatimaye kuna matumaini makubwa ya kurejea kwa hali ya utulivu nchini humo kutokana na nia ya EAC.

Makamu wa Rais Hussein Akol alisema kwamba pande zilizokuwa zikihasimiana Sudan Kusini zimekubali kutekeleza mkataba wa amani wa mwaka 2018 na kuhakikisha kwamba nchi hiyo ina amani na kuzisaidia nchi jirani zinazokumbwa na misukosuko.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button