Swahil Fashion kufanya Disemba 2 mwaka huu
JUKWAA la Mavazi nchini maarufu kama Swahili Fashion Week, kufanyika Desemba 2, hadi 4, mwaka huu katika ukumbi wa Parthenon/ Greek Hellenic Club barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwandaaji wa onyesho hilo Mustafa Hassanali amesema jumla ya wabunifu hamsini (50) wataonyesha vipaji vyao katika jukwaa hilo.
“Swahili Fashion Week kufikisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake.mwaka huu
linatarajia kuleta pamoja wabunifu wapatao 50 kutoka nchi za Afrika Mashariki.
“Lengo la kuendeleza tasnia ya ubunifu Afrika bado linabaki kuwa kipaumbele, kupitia jukwaa hili na mtandao wake mkubwa kwa watumiaji wa bidhaa za ubunifu wa Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla sasa wataona mbadala wa bidhaazinazoingizwa kutoka nje.
“Wakati wote tumekua tukitilia mkazo thamani ya bidhaa za ubunifu za Afrika kwa kuhamasisha dhana ya “Made in Africa” na kutengeneza bidhaa zenye hadhi ya kimataifa kwa misingi ya Kiafrika.”
“Tunahamasisha Watanzania kupenda kuvaa mavazi yaliyobuniwa na wabunifu wa hapa Tanzania (Made in Tanzania). Kwa kufanya hivyo tunakuza vipaji vyao na kuwafanya siku moja kutambulika kama wabunifu wakubwa ulimwenguni.
Kwa upande wake katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. KedmonMapana amesema Upendo unaanzia nyumbani na ndiyo dhumuni la kufanya haya ili kukuza tasnia hii ya ubunifu nchini.
“Jukwaa pia linawahimiza wabunifu wachanga kutumia jukwaa hili, ikiwa ni hatua moja wapo katika kukuza vipaji vyao vya ubunifu.”