Swali la Mbunge Musukuma kivutio bungeni

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘Musukuma'.

MBUNGE wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu ‘Musukuma’,  amekuwa kivutio leo baada  ya kunyoosha mkono bungeni na kuuliza swali kwa lugha ya Kingereza kwa mgombea ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala), Habib Mnyaa.

Kitendo cha Musukuma ambaye amekua akijinadi kuwa na elimu ya darasa la saba kunyoosha mkono, ukumbi mzima wa Bunge ulilipuka kwa shangwe wakimpigia makofi, shangwe ambazo zilimuacha hoi Spika wa Bunge, Dk.  Tulia Ackson na kujikuta naye akifurahi.

Alipopewa nafasi ya kuuliza swali, Musukuma alianza kwa kusema: “Thank you madame Speaker (Dk Tulia), for give me this chance, Mr Mnyaa I want to ask you one question, where are you, what did you do for last five years?” Swali hilo la Musukuma liliongeza shangwe kwa wabunge na wengine kumtunza noti za shilingi 10,000.

Advertisement

Hata hivyo, swali hilo halikueleweka kwa mgombea na Spika Dk Tulia, ambapo Spika alimuliza umeelewa swali?

Mnyaa: Sijaelewa mheshimiwa Spika

Tulia: Wabunge hebu nyamazeni tafadhali, Mheshimiwa Musukuma hebu rudia swali lako.

Musukuma: What did you do for last five?

Dk Tulia: Mgombea umeelewa?

Mnyaa: Sijaelewa Mheshimiwa

Dk Tulia: Ngoja nimsaidie, swali lake ameuliza ‘what did you do for past five years?

Akijibu swali hilo, Mnyaa amesema: “Nilikuwa nafanya kazi katika Bunge Eala kupitia kamati na nilifanya vitu vingi sana, nikishirikiana na wenzangu katika miaka mitano iliyopita. Nasimama mbele yenu nikiomba kura zenu