Swear kumshirikisha Ally Kiba

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, kutoka Kisiwani Zanzibar, Ally Swear amesema ana mpango wa kutoa ngoma mpya akimshirikisha Staa wa muziki kutoka Tanzania Bara, Ally Kiba.

Akizungumza na HabariLEO, msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa ‘Nakusubiri’ alisema sababu ya kumchagua¬† Kiba ni kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao katika kuimba.

“Kiba ni msanii ambaye ananivutia sana kuanzia saiti yake staili yake ya uimbaji ndio maana nikaamua kumchagua yeye,” alisema Swear.

Msanii huyo ameeleza kuwa tayari ameanza maandalizi ya ngoma hiyo ambayo anaamini hadi  kufikia mwishoni mwa mwezi Mei tayari itakuwa imekamilika.

Alisema hawezi kusema ataipa jina gani kwa sasa lakini anaamini itakapo kamilika atakuwa na jina sahihi la kuipa kutokana na mvuto itakaokuwa nao.

Endapo projekti hiyo itafanikiwa, Swear atakuwa ni miongoni mwa wasanii wachache kutoka Zanzibar kumshirikisha Ally Kiba ngoma zao.

Habari Zifananazo

Back to top button