Swift aweka rekodi Spotify

MSANII Taylor Swift kutoka Marekani amekuwa msanii wa kwanza wakike kufikisha wasikilizaji milioni 100 katika mtandao wa Spotify ndani ya mwezi.

Mwimbaji huyo ambaye ametoa mfululizo wa albamu mpya miaka mitatu iliyopita, bado yuko nyuma ya The Weekend, ambaye ana wasikilizaji wengi zaidi wa kila mwezi akiwa na wasikilizaji milioni 110.

Akitangaza hatua mpya, Swift aliandika kwenye mitandao ya kijamii: “Tabia ya malkia. Tarehe 29 Agosti, Taylor Swift amekuwa msanii wa kwanza wa kike katika historia ya Spotify kufikia wasikilizaji milioni 100 kwa mwezi.

Swift anatazamiwa kuachia ‘1989 (Taylor’s Version)’ kama albamu mpya iliyorekodiwa upya mnamo Oktoba 27, 2023, ambayo ni kumbukumbu ya miaka tisa ya 2014 LP.

Advertisement
4 comments

Comments are closed.