Swissport yajivunia faida mwaka 2022
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Swissport Tanzania, Mrisho Yassin amesema licha ya changamoto ya ugonjwa wa Uviko-19, bado kampuni hiyo ilifanya vizuri katika kukusanya mapato kwa mwaka 2022 kulinganisha na mwaka 2021, ambapo faida ilikua Sh bilioni 2.
1.
Amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa mwaka kati ya kampuni ya Swissport na wanahisa uliofanyika leo Mei 25, 2023 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mkutano wa 38 lengo likiwa kupitisha hesabu za kampuni na kufanya gawio kwa wanachama.
Amesema Kampuni ya Swissport imekusanya mapato ya Sh Bilioni 37 na kupata faida ya Sh bilioni 2.5 kabla ya kodi ya VAT, hivyo itatoa gawio la faida ya hisa kwa mwaka 2022, kwa wanachama wake.