Swissport yawapa gawio wanahisa

DAR ES SALAAM; Kampuni ya Swissport imetoa gawio la asilimia 51.3 sawa na Sh bilioni 1.8 kwa wanahisa wake.

Akizungumza Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Mrisho Yassin amesema gawio hilo limetokana na faida waliyoipata na kueleza kuwa  mwaka 2023 walipata faida ya Sh bilioni 3.6, hivyo katika Mkutano Mkuu wa wanachama waliamua kutoa gawio hilo.

“Mwaka 2022 kampuni yetu ilipata faida ya Sh bilioni 2.6 na mwaka 2023 ilipatikana Sh bilioni 3.6 ambayo ni ongezeko la asilimia 27 kwa hisa na faida,” amesema.

Amesema kampuni yake ambayo inahudumia mizigo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KIA), inatarajia kuongeza huduma hiyo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Aman Karume, na kile cha Mwanza lengo likiwa ni kuongeza mapato kwenye kampuni hiyo.

Akizungumzia kuongezeka kwa faida, Yassin amesema imechangiwa na filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwani watu wengi wanaingia nchini kupitia viwanja hivyo kutokana na filamu hiyo kuhamasisha utalii.

Habari Zifananazo

Back to top button