MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi amesema kuwa kazi ya uandishi wa Habari ni kazi ya taaluma kama zilivyo kazi nyingine.
Feleshi ameyasema hayo leo Juni 13, 2023 mara baada ya kuwasilisha muswada wa sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
Amesema, lengo la kufanya marekebisho katika vifungu tisa vya sheria hiyo ni kuifanya taaluma hiyo kuwa kama zilivyo vyingine.
Amesema muswada huo umeondoa mambo mengi ambayo yalikuwa kero kwenye sheria hiyo ikiwemo adhabu kubwa za vifungo na faini walizokuwa wakikabiliana nazo waandishi.
|Feleshi amesema kuwa licha ya kuwepo kwa ukomo wa baadhi ya mambo, lakini imetazama kwa kiasi kikubwa kada hiyo ili kuwafanya waandishi wawe huru katika utendaji kazi wa kila siku.