Taarifa ya mabadiliko yaduwaza wabunge

RAIS Samia Suluhu Hassan, leo amefanya mabadiliko madogo kwenye Baraza lake la Mawaziri.

Sasa ipo hivi wakati taarifa hiyo ikisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ndani ya Bunge ulikuwa unaendelea mjadala wa hoja ya Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Katiba ya Tume ya Usafiri wa Anga ya Afrika ya Mwaka 2009 iliyowasilishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

Lakini ilionekana kama baadhi ya wabunge walianza kupata taarifa kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea Ikulu cha kutangazwa mabadiliko na hata wale ambao wamepata uteuzi au wale waliobadilishwa nao walianza kuhisi joto fulani wakiwa ukumbini.

Advertisement

Wakati taarifa za mabdiliko zikizidi kusambaa, mjadala wa hoja ya Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Katiba ya Tume ya Usafiri wa Anga ya Afrika ya Mwaka 2009 ulikuwa ukielekea mwishoni, ambapo baadaye Bunge liliridhia Azimio hilo.

Baada ya kutoka nje ya ukumbi, baadhi ya wabunge walikuwa katika vikundi kupeana taarifa mbalimbali na wengine kuanza kutoa maoni yao, huku baadhi wakikataa kutoa maoni kwa maelezo bado walikuwa hawajapata taarifa kamili, kwani imekuwa kama ‘surprise’ kwao.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *