Taasisi ya Ansarullah Tanzania yaadhimisha siku ya Uhalifa

TAASISI ya Kiislam ya Majlis Ansarullah leo imeadhimisha siku ya Uhalifa ‘uongozi’ duniani katika ukumbi wa mikutano wa Masjid Salaam uliopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

SADR Majlis Ansarullah, Dk Swaleh Kitabu Pazi (kulia) akiwa katika kikao cha maadhimisho ya siku ya uhalifa duniani muda mchache baada ya kufungua kikao hicho katika ukumbi wa Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Akizungumza katika maadhimisho hayo SADR, Swaleh Kitabu Pazi alisema lengo la maadhimisho ni kuifanya jumuiya hiyo kuendelea kuwa na uongozi bora, nidhamu na kuheshimu viongozi katika ngazi mbalimbali.

Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, alipowasili kwa ajili ya kutoa hotuba katika maadhimisho ya siku uhalifa iliyofanya Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.

Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam Ahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akizungumza katika maadhimisho ya siku uhalifa iliyofanya Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo

SADR Pazi alisema waislam duniani kote wanahitaji uongozi kwa kuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu katika kuheshimu dhamana wanazopewa katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

Mmoja ya watoa mada wakiwasilisha historia ya uhalifa katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

“Huwa pia tunatoa huduma mbalimbali, tunafanya mahubiri, machapisho, magazeti, majarida, lakini pia kuwasaidia wasiojiweza kama watoto yatima, tuna mipango mingi tunafanya.” Alisema SADR Pazi.

SADR Pazi alisema huduma na misaada wanayoitoa imekuwa ikilenga pia na maeneo ya vijijini.

SADR Majlis Ansarullah, Dk Swaleh Kitabu Pazi akizungumza na HabariLEO katika maadhimisho ya siku ya uhalifa duniani katika ukumbi wa Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Naye, Naib Amir Sahib Shekhe Abdulrahman Mohammed Ame alisema taasisi hiyo imekuwa ikifanya huduma zake kwa mapato yatokanayo na michango mbalimbali ya watu wake ambao wamekuwa kipaumbele kufanya taasisi hiyo kuwa hai.

Wageni waliojitokeza katika kuadhimisha siku ya uhalifa duniani iliyofanyika ukumbi wa Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo

“Kila mwanajumuiya anatakiwa atoe 1/16 ya mapato yake, lakini kwa wenye nia zaidi wanatoa mpaka 1/3 ya mali zao na hayo mambo yanafanyika.” alisema Shekhe Ame.

Naib Amir Sahib Shekhe Abdulrahman Mohammed Ame akitoa hotuba katika maadhimisho ya siku ya uhalifa iliyofanyika ukumbi wa Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Amesema licha ya huduma za kiimani pia taasisi hiyo imekuwa ikitoa huduma zingine zikiwemo za maji, afya na umeme wa jua.

Naib Amir Sahib Shekhe Abdulrahman Mohammed Ame akizungumza na HabariLEO katika maadhimisho ya siku ya uhalifa iliyofanyika ukumbi wa Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Wageni waliojitokeza katika kuadhimisha siku ya uhalifa duniani iliyofanyika ukumbi wa Masjid Salaam Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo

Habari Zifananazo

Back to top button