Taasisi ya Mandela yatakiwa kupaa

TAASISI ya  Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) inatakiwa kupaa zaidi katika anga za juu kwenye tafiti na teknolojia kwa maendeleo ya nchi.

Akikabidhi kijiti kwa mkuu mpya wa taasisi hiyo aliyekuwa Makamu wa Rais ,Dk Bilal  na mkuu wa chuo hicho wa kwanza amesema taasisi hiyo ni iliyopo nchini ni imara.

“Natamani kuiona taasisi hii  ikipaa  zaidi katika anga za juu katika tafiti , bunifu na teknolojia na aliwapongeza watumishi wa taasisi hiyo kwakuhakikisha jina la NM-AIST linapaa ”

“Nimekuja hapa kwa sauti imara lakini ninahamu ya kuona taasisi hii inapiga hatua zaidi na najua mwenzangu Omari Issa ataiweka taasisi hii katika anga za juu zaidi.”

Mkuu wa taasisi hiyo, Omari Issa amemshukuru, Dk Bilal kwa utumishi wake chuoni hapo kwani uongozi wake mahiri umeleta mafanikio makubwa kutokana na juhudi zake binafsi kama kauli mbiu isemayo “taaluma kwa maendeleo ya viwanda”.

Habari Zifananazo

Back to top button