Taasisi ya Mkapa yajenga nyumba 50 watumishi wa afya

TAASISI ya Benjamin Mkapa (BMF), imejenga nyumba za watumishi wa afya 50 katika maeneo mbalimbali Mkoa Mtwara.

Ofisa Miradi Mwandamizi wa taasisi hiyo Dk Daudi Ole Mkopi, amesema nyumba hizo zimejengwa ndani ya miaka 17 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 2006.

“Kupitia taasisi yetu hadi leo, tumeweza kujenga nyumba za watumishi wa afya 50 katika mkoa wa Mtwara,” amesema.

Mbali na ujenzi wa nyumba hizo, BMF pia wamepatia mkoa jumla ya watumishi 192, ambao wanatoa huduma za afya katika hospital za serikali mkoani Mtwara.

Mkopi amesema hayo wakati taasisi hiyo ilipofika Kituo cha Afya cha Lupaso, Masasi mkoani Mtwara kukabidhi mashine ya maabara, ambayo imetolewa na taasisi hiyo kama msaada kusaidia kuimarisha huduma za afya kituoni hapo.

Msaada huo umetolewa kama sehemu ya kusherehekea miaka 17 ya uhai wa taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.

“Kama sehemu ya kusheherekea miaka 17 ya uhai wa taasisi, tumeona ni vyema kujumuika na wananchi hasa kwenye kituo ambacho kipo ndani ya ardhi ambayo hayati Benjamin Mkapa, muasisi wa taasisi hii kama sehemu ya kuendeleaza kuenzi maono yake kuwezesha uboreshaji wa shughuli za afya nchini,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button