Taasisi yapiga jeki huduma za afya

TAASISI ya Sukos Kova Foundation imetoa vifaa 15 vya kisasa vya kukusanya hewa ya oksijeni (Oxygen Concentrators and Oximeters) kwaajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye uhitaji wa huduma za dharura ikiwemo wahanga wa majanga nchini.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh milioni 16.6 vimetolewa kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Kamishina wa Polisi Mstaafu Suleiman Kova alisema vifaa hivyo ni muhimu hasa kwa uwezo wake wa kutengeneza oksijeni kwa kutumia umeme bila kuhitaji kujaza oksijeni upya.

Advertisement

“Kwa kutambua idadai kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali zetu tunaimani vifaa hivi vitatumika na uwezo mkubwa zaidi wa kutoa huduma kwa urahisi kutokana na uwezo wake ulioelezwa,”anasema Kova.

Amesema vifaa hivyo vitaleta ufanisi mkubwa na tija wakati wa kuwahudumia wagonjwa hasa waliomahututi. Ameipongeza Muhimbili kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika hospitali ili kuakisi mahitaji ya wananchi .

“Napongeza pia Wakurugenzi wa JKCI na MOI  kwa kazi nzuri inayofanywa katika Taasisi hizi hakika wadau wanaendelea kuhamasika kuunga mkono juhudi zao na wadau wengine wa maendeleo nchini kuunga mkono juhudi za kuboresha sekta ya afya kwa maslahi mapana ya Taifa letu,”amesema Kova.

Kova anaahidi kutoa misaada zaidi ya aina hiyo kwa kushirikiana na Taasisi Mwenza ya Peaceland kutoka China na kusimamia misingi ya uadilifu,weledi na kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza athari za majanga na maafa nchini Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *