Taasisi za serikali zapewa siku 90 kulipa madeni

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku 90 kwa mamlaka za serikali kulipa malimbikizo ya malipo ya huduma wanazopata kutoka kwa taasisi nyingine

Majaliwa ametoa agizo hilo bungeni Dodoma leo wakati anatoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 11 wa bunge la 12 ulioanza Aprili 4 mwaka huu.

Amesema, baadhi ya taasisi zimekuwa zikichelewesha malipo au kutolipia kabisa huduma wanazozipata kutoka taasisi nyingine za serikali zikiwemo huduma za maji, umeme, simu, pango na ujenzi.

Advertisement

“Ninazielekeza taasisi zote za serikali kulipia huduma wanazopata kutoka taasisi nyingine ikiwemo Shirika la Umeme (TANESCO), Shirika la Mawasiliano (TTCL), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Wakala wa Majengo (TBA) na Mamlaka za Maji ifikapo tarehe 30 Septemba 2023 ili kuepusha kukwamisha uendeshaji wa Taasisi hizo,” amesema.

 

1 comments

Comments are closed.