Tabaro: Msikatie tamaa watoto waliofeli kidato cha 4

DAR ES SALAAM: WAZAZI na Walezi wametakiwa kuacha kuwakatia tamaa na kuwanyanyapaa watoto ambao wamefeli kidato cha nne na badala yake wametakiwa kuwasaidia warudie mitihani ili waweze kutimiza ndoto zao kimaisha.

Hayo yamezungumza na Mkurugenzi wa shule huria ya Ukonga Skillfull Diodorus Tabaro katika mahafali ya 17 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo.

Amesema wazazi wengi wamekuwa kikwazo kwa watoto wao ambao wanafika shuleni hapo kujiandikisha kurudia mitihani lakini asilimia kubwa ya wazazi na jamii inayowazunguka huwabeza na wengi wao wanagoma kuwalipia ada ili waweze kurudia mitihani yao ya kidato cha nne.

“Hapa kuna wanafunzi ambao wanarudia mitihani tumekuwa tukiwasaidia, wazazi unakuta uwezo wa kulipa anao lakini hataki anasema kama alisoma miaka minne na akafeli mwaka mmoja atafaulu vipi? alisema Tabaro na kuwasha rekodi ya Rais Samia Suluhu Hassan akitoa historia yake kuwa hata yeye hakufanya vizuri kidato cha nne lakini alijiendeleza na sasa ni Rais.

“Mimi mama yenu nimetoka kwenye familia tu ya kawaida, baba yangu alikuwa mwalimu na mama yangu alikuwa mama tu wa nyumbani, sikusoma sana nilisoma mpaka kidato cha nne sikufanya vizuri, wakati sisi tunamaliza shule unapangwa unakwenda wapi, nikapangwa kwenda ofisi Kuu ya Maendeleo, nilikuwa na miaka 16 mwajiri akasema nirudi child labor (ajira kwa watoto)

“Mwaka uliofuata nikiwa na miaka 17 ndio wakaniita nimeanza ofisa masijala nilifanya kazi kwa miaka mitatu lakini kila nikifanya niliyowakuta nawaongoza mimi, nilisoma mazingira yaliyonizunguka na kujua mila na desturi ya taasisi ile,

“Nilihisi hapa nilipo sipo, nikaanza kujisomesha mwenyewe nikafanya kozi ya statistics (takwimu) ngazi ya cheti, nikamaliza nikafanya management(uongozi) ngazi ya cheti nikapandisha sifa nikaenda zangu Chuo cha ADM nikafanya Advance Diploma kwa miaka mitatu.

“Nikarudi ofisini nikawa afisa mipango nikaa miaka miwili zikatangazwa kazi Shirika la Mpango la Chakula Duniani (WFP) nikafanya miaka tisa nikarudi serikali, nikaona watu wanaenda ‘to slow’, nikachomoka nikaenda kwenye ma NGOs nikawa kiongozi taasisi changa , mwaka 2000 nikageukia siasa na sasa ni Rais.”

Baada ya kucheza rekodi hiyo ya Rais, Tabaro akasema watoto wengi wanaorudia mtihani wa taifa jamii ilishawapa mtazamo hasi, kwamba alishamaliza kidato cha nne akashindwa kwa hiyo anapoamua kurudi shule ule mtazamo toka ndani ya familia ni tofuati.

“Ndio maana maana wazazi wengi wanawapa kipaumbele watoto wanaonza kidato cha kwanza kwenye mfumo rasmi wanaorudia hawapewi kipaumbele,kiasi cha ada tunachotoza ni kidogo ni sh 650,000 kwa mwaka lakini unakuta mzazi anagoma kumlipia.

“Mtoto anatamani shule, anatamani kusoma mzazi hatoi ada, ukiangalia si kwamba mzazi hana uwezo anakwambia wewwe ulishafeli huna chochote.”Amesema.

Aidha, amesema shule ya Ukonga Skillfull ina wanafunzi wa aina tatu wapo ambao wapo kwenye mfumo rasmi wa elimu ambao ni kidato cha kwanza hadi cha nne, wapo ambao wanarudia mitihani yao ya kidato cha nne lakini pia wapo wanaosoma Qualifying Test ‘QT’

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
28 days ago

Mike, great work. I applaud your efforts enormously because I presently make more than $36,000 each month from just one straightforward online company! You may begin creating a steady online income with as little as $29,000, and these are only the most basic internet operations jobs.
.
.
Detail Here——————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

StaceyCanales
StaceyCanales
27 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 27 days ago by StaceyCanales
KUJENGA MILELE DAIMA
KUJENGA MILELE DAIMA
26 days ago

Kwa ajili ya UTABIRI WA URAIS WA 7, 8, 9…….. 50 …. NA KUKUONGEZEA KURA ZA URAIS (MSWALA UMECHAKAA)

CCM TUKIMALIZA SIASA ZA KUMSIFIA RAIS, KUJENGA BARABARA, KUJENGA HOSPITALI, KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA, NYUMBA ZA POLISI, SHULE, TUTAFANYA SIASA ZA AINA GANI?

KUMBE KUJENGA MILELE DAIMA

Capture.JPG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x