Tabora United wamtwisha mzigo kocha mpya

KOCHA mpya wa Tabora United, Dennis Laurent Goavec, atalazimika kuchukua Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kuifikisha nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kama mipango ya timu hiyo inavyomtaka.

Msemaji wa timu hiyo Christina Mwagala, amesema wanaamini kocha huyo atawafikisha nafasi nne bora za juu katika ligi, lakini pia watabeba kombe la shirikisho.

“Kwa kocha huyu tumelamba dume, wachezaji watamuelewa ufundishaji wake, tumepanga tushinde mechi zote 9 zilizosalia katika ligi, lakini pia tuchukue Kombe la ASFC maana nafasi na uwezo huo tunao,” amesema Mwagala.

Advertisement

Amemuelezea kocha huyo raia wa Ufaransa kwamba ana uzoefu wa soka la Afrika, ameshawahi kuifundisha timu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

/* */