TACRI yajivunia utafiti zao la kahawa Kagera

KAGERA: Taasisi ya utafiti wa zao la kahawa TACRI Kanda ya Kagera imeanza kujivunia mafanikio ya utafiti uliofanyika mwaka 2004 hadi 2011 juu ya aina nne za kahawa ya Robusta zenye ukinzani na ugonjwa wa mnyauko fizari ambazo zimetumiwa na wakulima wa kahawa bila kupata magonjwa yanayopunguza uzalishaji katika zao hilo.

Akizungumzia mafanikio ya utafiti Meneja wa kanda ya Kagera kutoka taasisi ya utafiti, Dk Nyabis Ng,homa amesema kuwa baada ya wakulima kuhangaika kwa muda mrefu kupambana na magonjwa ya mnyauko katika zao la kahawa sasa ni kicheko baada ya utafiti kufanikiwa kwa asilimia 100% mara baada ya wakulima hao kuanza kutumia aina ya kahawa zilizofanyiwa utafiti na kuanza kutumika mwaka 2016.

Amesema aina ambazo zilifanyiwa utafiti zimeonekana kutoshambuliwa na ugonjwa na wakulima kupata mavuno mengi kwa misimu ya mavuno ya kahawa mwaka 2021/2022 na msimu wa 2022/2023 huku akitaja aina hizo kuwa ni Maruku1, Maruku 2, Bukoba1 na Muleba 1 ambapo amedai kuwa kwa sasa aina hizo hazishambuliwi na magonjwa na zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katikauzalishaji wa zao la kahawa.

‘’Mkoa wa Kagera kwa miaka mingi umekuwa ukizalisha zao la kahawa kama sehemu ya kuinua uchumi, ingawa baada ya mnyauko fizari kushambulia mibuni wakulima wakakata tamaa ,lakini tasisi ya utafiti iko tayari kuwahudumia wakulima na kuwasaidia,baada ya aina iliyofanyiwa utafiti kuanza kutumiwa na wakulima tayari kuna mafanikio.”amesema Ng’homa.

Ametaja mafanikio mengine ya taasisi hiyo kuwa ni kutoa matokeo ya tija kuhusu mpangilio wa mashina ya kahawa ya Robusta,na mfumo wa kilimo mseto cha kahawa na migomba,kubaini vimelea vya ugonjwa wa kutu ya majani vinavyoshambulia kahawa ya Robusta, pamoja na kubaini aina nane za vinasaba vya kahawa ya Robusta kutoka kwenye makundi mawili yenye asili ya Kongo na Afrika Magharibi.

Hata hivyo amesema taasisi hiyo imetekeleza kwa ufanisi mpango wa serikali na mkakati wa kitafa wa uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa ulioanza kutekelezwa mwaka 2021/2022 ambapo kufikia Novemba 2023 jumla ya miche ya kahawa 19,336,574 imezalishwa na kusambaza kwa wakulima sawa na asilimia 77.35 ya lengo la kuzalisha miche 25,000,000 ifikapo 2025/2026.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button