TADB yampa nguvu mwekezaji Karagwe

KAGERA; Karagwe. BENKI ya maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), imetoa kiasi cha Sh bilioni 1.7 kwa ajili ya kununua ng’ombe mitamba 600, ili kuunga juhudi za mwekezaji wa kiwanda cha maziwa cha Kahama Fresh katika mradi wake wa kopa ng’ombe lipa maziwa, ili kuwawezesha vijana kujiajiri.

Mkurugenzi wa TADB ,Frak Nyabundege amesema serikali ilikuja na maono ya mradi wa (BBT), kwa sekta ya uvuvi na mifugo, lakini mwekezaji huyo akayatumia maono hayo kujenga kesho ya vijana wafugaji katika Wilaya ya Karagwe kwa kuwapa ng’ombe na wafugaji hao kulipa maziwa, hivyo nao hawana budi kuyakamilisha maono ya mwekezaji huyo.

“Sisi Kama TADB ni mfadhili pia kiwanda cha Kahama Fresh , baada ya kuona ndoto ya mwekezaji mzawa kwamba atawasaidia vijana kupata ajira kupitia ufugaji tukaona ni nafasi ya kipekee sisi kumuunga mkono bila kusubiri.

“Lakini hii ni fursa ya kipekee kwa vijana waliohitimu vyuo mbalimbali nchini kuhakikisha wanajiajiri kupitia ufugaji na baada ya vikundi kuimarika sisi kama benki ya kilimo tutaendelea kuvisimamia vikundi vya vijana,”amesema Nyabundege.

Mwekezaji huyo Jossam Ntangeki alitoa ng’ombe mitamba 5 kwa kikundi cha vijana 17 wafugaji wa Kata ya Kihanga wilayani Karagwe kama mfano kwa vijana wengine na ishara ya vijana walio tayari kubadilisha mtizamo kwa jamii ya mkoa wa Kagera kuwa vijana ni chachu ya maendeleo na suala la ufugaji sio la watu masikini.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abudalla Ulega amesema kuwa serikali inatarajia kumuongezea mwekezaji wa kiwanda cha Kahama Fresh eneo la kufugia katika ranchi ya Kagoma, ili kuendelea kuchochea masuala ya ufugaji bora, baada ya mwekezaji huyo kuendelea kufuga kwa tija na kufuata kanuni zote za mifugo katika maeneo aliyopewa na serikali.

Msajili wa Bodi ya Maziwa George Msalya amesema kuwa Tanzania ina viwanda vya kusindika maziwa 153, hivyo kiwanda cha Kahama Fresh kutafikisha jumla ya viwanda 154, huku akisema kuwa bado kuna upungufu mkubwa wa maziwa na kuvitaka vikundi vinavyopokea mitamba kujitahidi kufuga kwa tija ili kupata maziwa mengi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x