Tafiti saba kuboresha huduma za kibingwa nchini

ZAIDI wataalamu wa afya 150 wamekutana jijini Dar es Salaam leo kujadili tafiti saba za kuboresha huduma za kibingwa bobezi zinazopatikana nchini ikiwa ni hatua ya kuimarisha matibabu ya kibingwa na kutimiza azma ya tiba utalii nchini.

Kati ya tafiti hizo zilizojadiliwa nne zinatoka Tanzania huku tafiti tatu zikitoka Korea Kusini.

Akizungumza wakati uzinduzi wa kongamano la nne la kujadili tafiti ,Kaimu Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila ,Dk Faraja Chiwanga amesema wanalenga kuzipitia na kujadili tafiti ambazo zimekuwa zinafanyika pamoja na maendeleo katika sekta ya afya na utoaji wa huduma za kibingwa nchini.

“Sekta ya afya huwa inakua sana kutokana na maendeleo ya sayansi kwahiyo kila mwaka huwa tunaanda kongamano kujadili natumefanya kwa kushirikiana na African Future Foundation pamoja na KOFFI kutoka Korea Kusini na tumeshirikiana na chama cha madaktari wa tiba za ndani”.amesema Chiwanga.

Dk Chiwanga amesema mambo mengine yatakayozungumzwa ni jinsi sekta ya afya inavyokua  hasa katika kutoa huduma za bingwa bobezi kama inivyofahamika hivi karibu Muhimbili mambo mengi yamefanyika ikiwemo tiba za kibingwa ambazo zilikuwa  hazifanyiki nchini na Ukanda wa sahara .

Amesema wataalmu kutoka Korea Kusini wataeleza maendeleo yanayofanyika katika tiba bobezi ambayo pia yanaweza kufanyika hapa nchini  katika kuendelea kusimamia azma ya Serikali ya Tanzania katika kuongeza tiba bingwa bobezi na kufanya Tanzania iwe sehemu ya utalii wa tiba pamoja na kukuza uchumi hasa kwa kuongeza fedha za kigeni.

“Tumekuwa na wenzetu wa Chama cha Madaktari Tanzania wataeleza nafasi ya vyama vya kitalaamu  katika kuendeleza sekta ya afya,Katika mawasilisho wataonesha uwekezaji ambao umefanyika sekta ya afya  na mambo yanayofanyika hasa huduma za kibingwa zinazotolewa.

Amesema watajenga uwezo wa ndani wa  kutoa huduma za kibingwa ili wagonjwa kutoka nje waje kutibiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button