“Tafuteni masoko ya nje ,mtajionea wenyewe”

DAR ES SALAAM: Serikali kupitia kituo cha uwekezaji Nchini (TIC) kimewataka wazalishaji wa ndani kujikita katika tafiti za masoko ya nje ikiwemo ulinganifu wa bei ili kuona ni jinsi gani bidhaa hizo zitaweza kuingia katika soko shindani.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa bodi (TIC), Dk Binilith Mahenge wakati alipotembelea kiwanda cha Akbalish Hardware and electric kilichopo Pugu jijini Dar es salaam.

Amesema ni wazi kuwa serikali hutegemea zaidi takwimu katika masoko hivyo tafiti hizo zitasaidia  katika kupunguza kodi chechefu na kuleta ahueni kwa wazalishaji hao kwa maslahi mapana ya taifa.

Awali akielezea baadhi ya changamato mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Akbalish Hardware and Electric, Juzer Alibhai amesema licha uwekezaji huo lakini masoko ya ndani bado ni changamoto hivyo serikali inapaswa kuliangalia hilo kwa jicho la kipekee.

Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendelea na ziara yake katika Mkoa wa Dar es salaam kwenye viwanda mbalimbali lengo ni kujionea hali ya uzalishaji pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakumba na kuzifanyia kazi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button