GHARAMA za ujenzi wa bomba la gesi lililokamilika na kesho kuwa na uwezo wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimeongezeka na kufikia Dola za Marekani bilioni 1.33 (Sh trilioni 2.7).
zaidi ya miaka 5 iliyopita
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa ametaka maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama itumike kutoa elimu itakayosaidia kupunguza tatizo la utapiamlo linalosababisha udumavu.
MKUU wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Chrispin Meela amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Vijijini, Dominic Kweka kumchukulia hatua za kinidhamu Mtendaji wa Kijiji cha Kokomay Kata ya Kiru, Raphael John kwa tuhuma za kunyanyasa kijinsia wanawake.
MKUU wa Mkoa wa Kagera, John Mongella amesema anasikitishwa na kutotumika kwa Jengo la Ushuru na Forodha la Pamoja la Afrika Mashariki (OSBP), lililokamilika mwaka mmoja uliopita.
SERIKALI imeombwa kuajiri watu wenye taaluma ya sheria kwenye mabaraza ya ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi iliyopo kwenye maeneo mengi ya miji na vijiji.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa India kufuatia kifo cha mwanasayansi aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo, Dk Avul Pakir Abdulkalam (83), kilichotokea hivi karibuni.
MTANGAZA nia kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Wakili wa Kujitegemea, Emmanuel Makene amemshtaki Polisi mgombea mwenzake, Lusajo Mpambalaga baada ya kumtolea matusi wakiwa katika kampeni za ndani za chama hicho.
WAGOMBEA nafasi za viti maalumu udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Tarime mkoani Mara, viongozi wa Umoja wa Wanawake(UWT) ngazi ya wilaya na zaidi ya wanachama 100 wamepinga matokeo ya uchaguzi huo wa UWT uliofanyika Julai 22 mwaka huu.
UWEPO wa idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka nchi za maziwa makuu umeufanya mkoa Kigoma kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa katika uandikishaji wa wakazi wa mkoa huo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, hivyo kuwachanganya vichwa viongozi wa serikali mkoani humo.
SERIKALI mkoani Shinyanga imewaonya viongozi wa madhehebu ya kidini kutochanganya masuala ya imani na siasa kwa kuwachagulia waumini wao mgombea wa kumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao kwani hali hiyo inaweza kusababisha kuingiza nchi kwenye machafuko.