SERIKALI imeombwa kuajiri watu wenye taaluma ya sheria kwenye mabaraza ya ardhi ili kupunguza migogoro ya ardhi iliyopo kwenye maeneo mengi ya miji na vijiji.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa India kufuatia kifo cha mwanasayansi aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo, Dk Avul Pakir Abdulkalam (83), kilichotokea hivi karibuni.
MTANGAZA nia kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Wakili wa Kujitegemea, Emmanuel Makene amemshtaki Polisi mgombea mwenzake, Lusajo Mpambalaga baada ya kumtolea matusi wakiwa katika kampeni za ndani za chama hicho.
WAGOMBEA nafasi za viti maalumu udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Tarime mkoani Mara, viongozi wa Umoja wa Wanawake(UWT) ngazi ya wilaya na zaidi ya wanachama 100 wamepinga matokeo ya uchaguzi huo wa UWT uliofanyika Julai 22 mwaka huu.
UWEPO wa idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka nchi za maziwa makuu umeufanya mkoa Kigoma kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa katika uandikishaji wa wakazi wa mkoa huo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, hivyo kuwachanganya vichwa viongozi wa serikali mkoani humo.
SERIKALI mkoani Shinyanga imewaonya viongozi wa madhehebu ya kidini kutochanganya masuala ya imani na siasa kwa kuwachagulia waumini wao mgombea wa kumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao kwani hali hiyo inaweza kusababisha kuingiza nchi kwenye machafuko.
IMEELEZWA kuwa Uchumi wa Tanzania umekuwa ukishuka mara kwa mara na kufanya fedha kushuka thamani kutokana na wawekezaji wengi wanaowekeza katika masoko ya hapa nchini kuweka fedha zao katika benki za nchi za nje.
OFISI ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Kaskazini imeipatia Hospitali teule ya mkoa wa Manyara msaada wa mablangeti 190 na mashuka 190. Mkurugenzi wa PPF Kanda ya Kaskazini, Onesmo Luhasha alisema juzi vitu vyote hivyo vina thamani ya Sh 6,650,000.
ASASI za kiraia nchini zimetakiwa kuwa ni wakala wa kutangaza amani, upendo na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
KAMPUNI ya Bima ya UAP Tanzania jana ilizindua huduma zake mpya, ambazo ni UAP Jikinge na UAP Family Kinga. Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond Komanga alisema huduma hizo, zinasaidia zaidi kwa walioathirika katika ajali na matatizo mengine.