VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba waliokuwa wakilalamikiwa na wagombea watatu David Jairo, Juma Killimbah na Amon Gyunda, kwa madai ya kumbeba Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni, wamehamishwa kwa muda ili kupisha mchakato kuendelea kwa amani na utulivu.