MABALOZI kutoka Umoja wa Ulaya (EU) wameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi, inayofadhiliwa na umoja huo na wameahidi kuongeza misaada yao zaidi kwa mkoa wa Kigoma.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agnes Kijazi amesema mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa ambayo yanatokana na mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa changamoto kubwa kwa wataalamu wa hali ya hewa nchini.
MKUU wa wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Festo Kiswaga, amesema serikali ya mkoa inatambua juhudi zinazofanywa na taasisi za dini kuleta maendeleo ya jamii katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya afya, elimu na maji.
WAKATI siku za kupiga Kura ya Maoni zikikaribia, imebainika kuwa zaidi ya nusu ya Watanzania wataipigia kura ya Ndiyo Katiba Inayopendekezwa.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ufafanuzi kuhusu suala la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura na siku maalum ya kupiga kura.
SIKU chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kutaka uangaliwe uwezekano wa kushusha nauli za vyombo vya usafiri nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema inatekeleza agizo hilo na kwamba nauli za daladala na mabasi ya mikoani zitashuka wakati wowote kuanzia sasa.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imependekeza kwa Serikali iongeze adhabu ya faini kutoka Sh milioni tatu na kifungo kisichopungua miezi sita na kuwa faini ya Sh milioni tano na kifungo kisichopungua miezi sita kwa wale wote watakaotuma katika mtandao taarifa za uongo.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa hati ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma anayekabiliwa na kesi ya kupokea Sh milioni 323.4, kwa kuwa hajafika mahakamani.
RAIS wa Umoja wa Vijana wa Afrika (PYU), Francine Mayumba amewataka viongozi wa nchi barani Afrika kuwapa nafasi vijana za kufanya mambo mbalimbali ya maamuzi kutokana na umuhimu wao katika jamii.