SERIKALI imekanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi, inayosema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa marais watano wa Afrika wanaolipwa mishahara minono barani Afrika.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
LICHA ya idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam, kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa Biometric Voters Registration (BVR), hali bado ni tete.
SASA ni rasmi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anajiunga katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na leo anatarajiwa kuzungumzia suala hilo, lililotanda katika siasa za Tanzania tangu baada ya kutopata nafasi ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wake wa urais.
WAGANGA wa tiba za asili nchini wametakiwa kujisajili na kupata vitambulisho kutoka serikalini ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa uhuru na kuwadhibiti matapeli.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, amewataka watendaji wa chama hicho kutozifunga ofisi zao, ili kutoa fursa kwa wanachama wa chama hicho kufanikisha mahitaji yao ya msingi hasa kipindi hiki cha mchakato wa kuwapata wana CCM watakaokiwakilisha chama katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
JUMLA ya wanafunzi 2,933 katika shule za msingi mkoani Shinyanga hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini kwenda Australia ambako leo anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne.
MKURUGENZI mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Kombwey aliyeapishwa juzi na Rais Jakaya Kikwete ameahidi uchaguzi huru na wa haki na kwamba utafanyika kwa wakati uliopangwa.
VIONGOZI wa madhehebu ya dini mkoani Morogoro wamewaomba watanzania waendelee kudumisha amani iliyopo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na kuwataka viongozi watakaochaguliwa kudumisha amani.
MUUNGANO wa Taasisi zinazoshughulikia maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (ZNCDA) umeishauri Serikali na Mashirika wahisani kuelekeza nguvu zao katika mapambano dhidi ya maradhi hayo kwa vile hivi sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya wananchi kuliko maradhi mengine yoyote Zanzibar.