WATANGAZA nia watatu kati ya wanne wanaogombea Jimbo la Iramba mkoani hapa, wametangaza kugombea mchakato wa kura za maoni wakidai kuwa mgombea mwenzao Mwigulu Nchemba 'anabebwa' ashinde.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
RAIS Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo na Taasisi ya African Achievers Awards, yenye makao makuu Afrika Kusini, kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha, kuendeleza na kudumisha Utawala Bora, kwa miaka 10 ya uongozi wake.
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), limetishia kufungua kesi dhidi ya wamiliki wa magari watakaogoma na kusababisha usumbufu kwa wasafiri.
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amewakumbusha watendaji wakuu wa serikali kutanguliza mbele amani na usalama wa nchi wakati wa uchaguzi mkuu ili uwe huru na wa haki, hatua itakayoendeleza sifa ya Tanzania.
MJUMBE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kamati ya Siasa, Kata ya Milanzi, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Didas Mwanisenga amekufa papo hapo huku wajumbe wengine 11 wakijeruhiwa wakati gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Hiace lilipotumbukia kwenye korongo.
CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinatarajia kudahili wanafunzi 10,000 mwaka huu kutoka jumla ya wanafunzi 8,600 iliodahili mwaka uliopita. Ongezeko hilo linatokana na chuo hicho kuwa na nafasi nyingi na kubwa za masomo kwa vitendo ili kutoa wataalamu walioiva katika tasnia ya kilimo , hifadhi na mifugo.
WATENDAJI mbalimbali wametakiwa kuacha tabia ya kuficha takwimu za wanafunzi waliobainika kuwa na mimba wakiwa shuleni, jambo ambalo linaweza kuchangia tatizo hilo kutoshughuliwa ipasavyo na hivyo kuendelea kurudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora imezindua rasmi ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Imalamakoye kilichoko katika kata ya Imalamakoye wilayani humo ili kumaliza kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa kijiji hicho na vitongoji vyake.
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Justin Nyari, jana aliwaeleza wakazi wa kata ya Levolosi jijini Arusha kuwa hawapaswi kubahatisha wakati wa kumteua mgombea wa chama hicho katika nafasi ya Ubunge kwani yeye ndiye mgombea pekee mwenye sifa za kulikomboa jimbo hilo.
MBUNGE wa Jimbo la Tarime anayemaliza muda wake, Nyambari Nyangwine, amedai kuchezewa rafu akisema kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakinywa pombe aina ya viroba kwa ajili ya kumzomea ili aonekane hakubaliki kutetea nafasi yake.