UCHAGUZI wa mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umevurugika na kuahirishwa, baada ya wagombea kutuhumiana kwa rushwa, huku watano wakikamatwa wakitoa kati ya Sh 15,000 na 20,000, kwa wajumbe wawachague.