SERIKALI ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka 2025 ambao unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude ameipongeza Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusogeza mbele upigaji wa kura za maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Taifa lolote linalotaka kuwa na amani na utulivu lazima liwekeze katika kuhimiza vijana kumcha Mungu.
WATANZANIA wametakiwa kuilinda na kuikumbatia amani kutokana na vitendo vya kigaidi na mauaji ya kutisha.
MADEREVA wa malori na mabasi yanayofanya safari za ndani na nje ya nchi, wametishia kugoma kufanya kazi kuanzia Ijumaa ijayo, ikielezwa ni kutaka kuishinikiza serikali kutatua changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za usafiri nchini.
PAROKO wa Kanisa Katoliki (RC) , Parokia ya Masasi jimbo la Tunduru-Masasi mkoani Mtwara, Dominick Mkapa amekemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watu waliopewa mamlaka serikalini mazingira yanayochangia kuwepo kwa mikataba mingi isiyo na tija kwa taifa letu.
TRENI mpya ya kisasa (Deluxe) ya Kampuni ya Reli nchini (TRL) imetajwa kuwa ni miongoni mwa treni iliyozingatia viwango vya kimataifa vya usafiri huo.
WATOTO 109 wamezaliwa katika usiku wa kuamkia sherehe za Pasaka katika hospitali za Amana na Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
MCHUNGAJI Bosco Maliga wa Kanisa la EAGT Majohe mji mpya Dar es Salam amewataka Watanzania kuyaogopa kama ukoma makundi ya watu wanaowapigia kampeni watu wengine ili wachaguliwe kuwa viongozi.
JESHI La Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeimarisha ulinzi katika kukabiliana na viashiria vya matukio ya kihalifu na ujambazi kwa kufanya doria ya helikopta katika mkoa huo na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani, katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka.