VIJANA wa kujitolea wanaomaliza mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wataendelea kuajiriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mikakati yake ya kukabiliana na ujangili katika hifadhi zake za Taifa.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
WATU 35 wakazi wa kitongoji cha Iroba kisiwani Bwiro wilaya ya Ukerewe, Mwanza hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao 13 kuchomwa moto katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.
KIKAO cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Iringa kimeunda timu maalumu itakayokutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete kuomba barabara ya Iringa mjini hadi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ijengwe kwa kiwango cha lami kabla ya awamu ya nne kumaliza muda wake.
WATU wenye uwezo kiuchumi wametakiwa kujenga utamaduni wa kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwamo ukarabati majengo na miundombinu mingineyo ya shule au vyuo walikosomea, ili iendelee kuwepo katika hali ya kupendeza.
WANANCHI katika kata ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, wameyakimbia makazi yao kwa ajili ya kukwepa kukamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutuhumiwa kuchoma nyumba tano za mtu anayedhaniwa kuwa ni jambazi sugu.
JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu sita wakazi wa kitongoji cha Ilolesha katika kijiji cha Madibila kata ya Mambwekenya wilayani Kalambo.
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanya kazi (TUCTA) limesema kutokana na madai ya walimu yakiwamo malimbikizo ya fedha za likizo na kupandishwa madaraja kuwa ya muda mrefu, wameamua kila wilaya waende kudai wenyewe kwa wakurugenzi wao.
WATU saba wanahofiwa kufa maji na wengine 49 wameokolewa kutokana baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kukumbwa na dhoruba katika eneo la vijiji vya mwambao wa kusini wa Ziwa Tanganyika.
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema hakuna kundi au mtu mwenye uwezo wa kuipindua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) au ile Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na atakayethubutu kuwaza au kupanga jambo hilo atakiona cha moto.
MWANAMKE Caseline Mzee (75) mkazi wa kijiji cha Guta wilayani Bunda, mkoani Mara, ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kunyongwa na kisha mwili wake kutupwa ndani ya mto, ukiwa umefungiwa mawe mazito ili usielee.