SAKATA baina ya Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Singida Vijijini limechukua sura mpya baada ya kikao cha Baraza la Jumuiya hiyo kuazimia kuitisha mkutano mkuu ili kumjadili.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete amesema katika mwaka huu Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), itaendelea kujikita katika kuelimisha jamii kuzuia na kudhibiti mimba za umri mdogo hususani kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri, ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatoa takwimu ya vyumba vya madarasa walivyobadilisha matumizi yake na kuvifanya vyumba vya maabara.
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amesema leo atakuwa na mkutano utakaompa hali halisi ya utekelezaji wa agizo alilotoa la kutafutwa kwa mtoto wenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel (4) aliyetekwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Ndamiwilayani, Kwimba mkoani hapa.
WATANZANIA wametakiwa kutumia fursa na haki iliyopo mbele yao ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki siku ya kura ili waachane na malalamiko ya kupatikana kwa viongozi mizigo.
NAIBU Waziri wa Maji, Amos Makalla ametaka bodi za wakurugenzi za mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini, kuweka vipaumbele vya ujenzi wa miundombinu ya majitaka na kuyaondoa maji taka yaliyotumika majumbani.
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imefuta ada ya wanafunzi wa shule za msingi, ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya mapinduzi ya kuwapatia wanafunzi wote elimu bure, kama ilivyoasisiwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume.
KAMPUNI tatu zimewasilisha ombi la kupigwa mnada kwa jengo la Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kufidia deni la dola za Marekani 1,182,595 ambazo zinadai shirika hilo.
RAIS Jakaya Kikwete ambaye ni mara yake ya mwisho kuhudhuria sherehe hizo, akiwa na wadhifa huo, aliteka umma uliokuwa uwanjani hapo, kutokana na kupokewa kwa shangwe na vigelegele alipowasili.
MAKUNDI mbalimbali jana yalipamba kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa maandamano sanjari na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali.