KAMATI ndogo ya Bunge ya Hesabu za Serikali imeitaka Wizara inayohusika na Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) kumuondoa na kumshusha cheo Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Nkasi, Deogratias Mboya.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MKAZI wa mtaa wa Kitianjala mkoani Arusha, Efatar Molel (45) anatarajiwa kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga leo(kesho) kwa tuhuma za kusafirisha milipuko isivyo halali.
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM wanakutana leo katika ukumbi wa makao makuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa chini ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
KAMATI ndogo ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kufuatilia na kuhakikisha Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) analipa deni la zaidi ya Sh milioni 750 analodaiwa na halmashauri hiyo.
WAKATI Taifa likielekea katika kura ya maoni ya Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu, viongozi wa dini nchini wametakiwa kutumia muda wao kuliombea taifa kuwa na amani na kulivusha salama katika matukio hayo makubwa.
MKE wa Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) nchini, Celine Mpango amewataka wanawake wa Afrika kutambua kuwa jukumu la kuwafuatilia wasichana katika maendeleo ya nchi ni la kwao na kamwe wasikubali kuwaacha nyuma.
WIMBI kubwa la kuwa na vijana wasiokuwa na kazi limeelezwa kuwa tatizo duniani kote na serikali mbalimbali zinatakiwa kuliangalia hilo kwa undani na kulitatua.
HALMASHAURI ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora imempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa jitihada na dhamira yake ya dhati ya kupambana na umaskini hapa nchini kupitia mpango wa kuzinusuru na kuziwezesha kaya masikini kiuchumi.
WATUMISHI wa idara, taasisi, mashirika mbalimbali ya serikali na binafsi wameshauriwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma na kupitia sheria na kanuni za kazi kabla ya kudai haki zao.
WAKAZI na wafanyabiashara wilayani Mkinga wameshauriwa kuanza kuona umuhimu wa kuwekeza ujenzi wa majengo hasa ofisi za huduma mbalimbali na makazi ya kupangisha ili kupunguza uhaba uliopo sasa.