WATU 18 wamekufa papo hapo kwa kuteketea kwa moto na wengine 11 wamejeruhiwa vibaya kutokana na basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso, katika kijiji cha Msimba tarafa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro – Mbeya.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
ASKOFU Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amesema yeye si tajiri kama inavyodhaniwa, bali alichonacho ikiwa ni pamoja na nyumba, magari na helikopta ni baraka tu za Mungu, lakini kama ni utajiri, anatarajia siku moja utamshukia.
WATANZANIA wengi wametajwa kuingia na kuishi nchini China kinyemela na kusababisha wanapopata matatizo yanayohitaji msaada wa serikali kushindikana kupewa, kwa kuwa hawamo katika utaratibu wa Diaspora.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Watanzania waishio ughaibuni hawataweza kupiga kura wakiwa nje ya nchi kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa sababu kuna mambo kadhaa ambayo Serikali inabidi iyatekeleze kabla ya kufikiwa kwa hatua hiyo.
JUMLA ya walimu wa shule ya msingi 18,000 kutoka mikoa 14 nchini, leo wanaanza mafunzo yenye kulenga kuwajengea uwezo wa kufundisha Mtaala mpya wa Elimu ya Msingi Darasa la I na la II.
POLISI katika Mkoa wa Kaskazini Unguja wamezuia mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao ulikuwa ufanyike katika Jimbo la Kitope kwa maelezo kuwa haukupata kibali cha jeshi hilo.
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto anatarajia kuanza ziara ya siku moja mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwa mikoa 10 nchini.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ametembelea baadhi ya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliojeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu wasiofahamika.
KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Gide, jijini Dar es Salaam limeandaa kitabu maalumu kuhusu msichana ambacho pamoja na masuala mengine, kinalenga kumwepusha na vishawishi na kumpotezea dira ya maisha.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuwalinda wawekezaji wenye leseni wanaofanya utafiti wa madini wa hapa nchini ili waanze uzalishaji mara moja.