SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuwalinda wawekezaji wenye leseni wanaofanya utafiti wa madini wa hapa nchini ili waanze uzalishaji mara moja.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura ambalo litaanza kuandikisha wapiga kura wapya mapema mwezi ujao.
MWENYEKITI wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa kwa kusimamia vyema maandalizi na kufanikisha maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
SERIKALI imesema ajira za walimu wapya zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu huku ikiweka wazi kuwa walimu hao wasitegemee kupangiwa katika maeneo ya majiji, manispaa na miji.
MAELFU ya wakazi wa Tarafa ya Kidatu wilaya ya Kilombero na Mikumi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro, walijawa na simanzi kubwa zilizotawaliwa na vilio wakati wa maziko ya miili ya watu 15 waliozikwa jana kwenye kaburi moja, ikiwa ni siku moja baada ya kufa kwa kuteketea kwa moto baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Nganga Express kulipuka lililopogongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso.
KUTOKANA na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria nchi nzima uliofanyika Ijumaa iliyopita, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilikuwa limeshaandaa mabasi 300 ambayo yangetumika kusafirisha abiria, imebainika.
RAIS Jakaya Kikwete amesema hajaletewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya maalbino nchini kwa sababu safari ya kisheria ya majina hayo kufikishwa kwake ni ndefu.
SERIKALI imesema inafuatilia kwa karibu maelezo yanayotolewa na Mtanzania Rashid Mberesero (20) aliyekamatwa Kenya akidaiwa kufanya ugaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa uliosababisha vifo vya watu 148.
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiungana na Watanzania kuomboleza vifo vya watu 19 walioteketea katika ajali ya basi lililoungua moto baada ya kugongana na lori juzi mjini Morogoro, imefahamika kuwa, ajali za barabarani zimegharimu maisha ya watu 969 kati ya Januari Mosi na Aprili 12 mwaka huu.
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kampala International University kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, wamefanya fujo na kuvunja viti, vioo na samani zingine za chuo hicho, ikiwa kama njia ya kushinikiza kutatuliwa kwa matatizo yanayowakabili.