KATIKA kuhakikisha inaondoa kabisa tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika nchini, Serikali imefanya mabadiliko ambapo kuanzia sasa mtoto wa darasa la pili hawezi kuruhusiwa kuingia darasa la tatu kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuondoa tatizo la watoto wanaomaliza shule ya msingi wakiwa hawajui kusoma.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
POLISI mkoani hapa imewatia mbaroni watu zaidi ya tisa wanaojihusisha na uhalifu wakiwa na milipuko hatari na zana za milipuko, wakiwa wamefichwa ndani ya Msikiti wa Suni kata ya Kidatu, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.
SERIKALI ya Tanzania inatarajia kufungua ubalozi nchini Kuwait kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha wa 2014/2015.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza kushusha nauli za mabasi ya Masafa Marefu huku ikiacha kabisa kuzigusa nauli za mabasi katika miji mikubwa, maarufu kama daladala.
ANAWAKE nchini wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ngazi ya udiwani na ubunge, kwani wana uwezo wa kuchochea maendeleo katika maeneo yao.
VIJANA wilayani Nachingwea mkoani Lindi wameamua kuhamasishana kwa kutoa elimu ya uraia na umuhimu wa upigaji kura kwa wananchi hasa wanawake na vijana, ili wajitokeze katika upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watendaji wa Serikali wilayani Kyerwa mkoani Kagera wameishauri na kuiomba Serikali kuboresha na kuongeza vitendea kazi ikiwemo magari ya Polisi kwa ajili ya kufanyia doria ili kudhibiti magendo ya rasilimali za nchi zinazovushwa na baadhi ya Watanzania wasiokuwa wazalendo.
MWANAFUNZI wa darasa la sita shule ya msingi Uhuru, Manispaa ya Arusha, Angel Gerald Mlay (12), Mkazi wa Sokoni One, anatafutwa na wazazi wake, baada ya kutoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha tangu Jumatatu wiki hii.
JUMLA ya watetezi wa haki za binadamu 450 na waandishi wa habari 100, wamepewa mafunzo maalumu ya mwenendo wa kazi zao na usalama nje na ndani ya maeneo yao ya uwajibikaji.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inakusudia kuanzisha adhabu za papo kwa hapo kwa ajili ya kudhibiti makosa ya barabarani ambayo baadhi yanafanywa na madereva kwa uzembe na kusababisha madhara makubwa.