WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amejiuzulu nafasi yake kutokana na kile alichosema ni kuandamwa kila kona kuhusu sakata la Akaunti ya Escrow huku akisisitiza kuwa yeye hahusiki hata kidogo na kashfa hiyo.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
“MIMI najiona kuwa na bahati kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete kuniamini na kuniteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, hasa kutokana na urafiki imara, mzuri na wa kindugu kati ya nchi hizi mbili,” ndivyo anavyoanza kueleza Balozi Shamim Nyanduga.
IMEELEZWA kwamba vijana wengi waliomaliza vyuo nchini, hawapati ajira kutokana na kutokuwa na ujuzi mbalimbali unaotakiwa na sekta binafsi.
KAMPUNI za simu za mkononi nchini zimeombwa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wakazi wa kata ya Ukata katika halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ili kurahisisha mawasiliano na kukuza uchumi wa eneo hilo.
MKAZI wa Gongo la Mboto, Francis Festo (38) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo akikabiliwa na mashitaka ya wizi wa pikipiki yenye thamani ya Sh milioni 1.7.
BALOZI za Japan na Sweden nchini, zimekubali kulisaidia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kupata vifaa vya maabara vyenye ubora na vinavyo endana na wakati.
MAHAKAMA ya Mwanzo Kariakoo, imemhukumu kifungo cha miezi sita nje, Sijali Mabiso (35) mkazi wa Kigogo, baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh milioni 2.2 kwa njia ya utapeli.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu amekitaka Kituo cha Uwekezaji (TIC) kuanzisha vyanzo vingine vya mapato ili kiweze kutekeleza miradi yake kwa wakati bila kutegemea bajeti ya serikali.
MWENDESHA pikipiki ameuawa na watu wasiofahamika kwa tumbo lake kutatuliwa na visu hadi utumbo ukatoka nje na mwili wake kutelekezwa eneo la makaburi ya Ipuli mjini Tabora .
WAKATI matumizi ya teknolojia yakielezwa kuongezeka katika nchi za Afrika hasa ya simu, Watanzania wameshauriwa kutumia simu zenye viwango vya kimataifa ili kuepukana na athari za matumizi ya simu bandia.