RAIS Jakaya Kikwete, amefanya mabadiliko muhimu katika Baraza la Mawaziri, kuziba pengo lililoachwa na mawaziri wawili, kutokana na kashfa ya utoaji wa fedha katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu (BoT).
zaidi ya miaka 5 iliyopita
HATIMAYE baada ya kukabiliwa na shinikizo la muda mrefu kuanzia katika vyombo vya habari, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye katika vikao vya vyama vya siasa, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amejiuzulu wadhifa huo.
MWENYEKITI wa kitongoji cha Songambele katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi kupitia chama cha ACT, Richald Madirisha (31) ameuawa kwa kuchinjwa na kiwiliwili chake kutenganishwa akituhumiwa kunyang’anya mke wa mtu.
ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema pamoja na kujiuzulu, ameiachia Shirika la Umeme (Tanesco), miradi ya kuongeza uzalishaji umeme, ambao ni muhimu katika kuifanya nchi kuwa ya kipato cha kati miaka kumi ijayo.
WAZIRI mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amesema ni vigumu kupata mwekezaji mzawa katika kazi za uchimbaji wa gesi, kwa kuwa kazi hiyo ni gharama kubwa duniani na kampuni za uchimbaji gesi hazizidi kumi.
ASASI inayoshughulika na Mambo ya Takwimu (OSSO) imeonya kuwa kitendo cha Serikali kutegemea fedha za wahisani kuwezesha ukusanyaji wa takwimu za ndani ya nchi ni hatari kwa taifa, kwani kunawapa fursa wahisani hao kujua mipango yote ya nchi.
TAASISI inayoshughulika na mambo ya Utafiti wa Kupunguza Umasikini (Repoa) ni miongoni mwa taasisi nne za Tanzania ambazo zimeorodheshwa kwenye ripoti ya dunia kuwa ni taasisi zinazofanya vizuri katika masuala ya utafiti, ufuatiliaji na ushauri.
MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imefungia mabasi mawili ya Kampuni ya Ibra Line Limited, yanayofanya safari za Dar es Salaam-Arusha na Moshi-Arusha, kwa kutoza nauli zaidi, kuongeza na kufupisha ruti kinyemela.
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Masha Musomba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.