WAISLAMU wametakiwa kuwa na subira wakati viongozi waliopewa dhamana ya kulifuatilia suala la Mahakama ya Kadhi wakifuatilia majibu.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
KAMATI ya Tanzania Kwanza, Nje ya Bunge Maalumu la Katiba, imesema ina imani na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene na kwamba ataimudu wizara hiyo.
JUKWAA la Katiba nchini (JUKATA) limesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa taifa, ipo haja ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupimwa afya zao na kutangazwa kwa wananchi ili kuepuka kuwaweka wagonjwa madarakani.
TAKRIBANI Sh bilioni 9.06 zinatarajia kutumika katika kupambana na tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Mbeya na Njombe.
BALOZI wa India nchini, Debnath Shaw amesema kuwa nchi yake itaendelea kuimarisha uhusiano uliopo na Tanzania katika kuhakikisha nchi zote zinafaidika na miradi mbalimbali ya maendeleo.
TAASISI ya Kimataifa inayojishughulisha na Usafirishaji, Uchukuzi na Uhudumiaji wa Bidhaa (CILT Africa) imeandaa Mkutano wa Kimataifa utakaowashirikisha wadau kutoka mataifa mbalimbali duniani utakaojadili masuala mbalimbali ya maendeleo na kufanyika jijini Arusha.
MJANE wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Mama Graca Machel ameiasa jamii ya Wakurya kuzingatia haki ya mtoto wa kike kupata elimu pamoja na kuachana na mila potofu ya ukeketaji.
LICHA ya wananchi kuunga mkono juhudi za serikali za kuchangia michango ya fedha za ujenzi wa nyumba za walimu, walimu wanne wanaofundisha shule ya msingi Mgongolo wilayani Igunga mkoani hapa bado wanaishi kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji zaidi ya miaka miwili sasa.
CHAMA cha Wananchi -CUF kimeamua kuahirisha maandamano yake, yaliyopangwa kufanyika jana, ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 14 ya vifo vya wafuasi wake waliopoteza maisha Januari 27, mwaka 2001.
MKAZI wa Mabwepande, Salome Muhando ambaye alitelekezwa na mumewe, baada ya kujifungua watoto sita, hatimaye amenunuliwa na kukabidhiwa nyumba na Benki ya Covenant ambayo ataishi yeye na wanawe.