USHIRIKIANO wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi bungeni, umemuomba Rais Jakaya Kikwete kuelekeza nguvu zake kwenye suala la umeme ili wananchi wapate nafuu ya maisha.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
WAKAZI wa Mtaa wa Njedengwa West , kata ya Dodoma Makulu wametishia kufanya maandamano makubwa kushinikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa huo Dennis Said aweze kukabidhi daftari la ugawaji wa viwanja kwa Mwenyekiti aliyechaguliwa kihalali na wananchi wa mtaa huo Pascal Matula.
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, limesema kwamba litaingia ubia na asasi ya Maendeleo ya Wanawake wa Kimaasai (Mwedo) ili kuimarisha mradi wa kijiji cha dijitali cha Ololosokwan.
KIJANA ambaye hakufahamika jina anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa katika eneo la kambi ya Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kata ya Nshambya mkoani Kagera.
WATU wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha Kibambila wilayani Kakonko mkoa wa Kigoma wamekufa na mtu mmoja amenusurika kifo kutokana na kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
MKUU wa Mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila ameonya askari Polisi katika mkoa huo, kuwa endapo watabainika kufanya vitendo vya uonevu dhidi ya raia na kuwanyanyasa, watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mtwara ni miongoni mwa halmashauri zilizonufaika na mpango wa kurasimisha rasilimali (Ardhi) na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA), mpango uliotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2011/2012.
VIJANA wawili wa kiume wenye umri wa miaka 16 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa kwa kosa la kuvunja nyumba ya askari polisi na kumuibia DVD yenye thamani ya Sh 70,000.
NAIBU Meya wa Halmashauri ya Mji wa Arusha, Prosper Msofe amekana kuwania ubunge jimbo la Arusha Mjini.
IMEELEZWA kuwa sehemu kubwa ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu imekwama au kutofanyika kwa wakati kutokaa na kuchelewa kwa ruzuku.