WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan amesema Katiba Inayopendekezwa sasa imezipatia ufumbuzi wa moja kwa moja kero za Muungano zilizokuwepo awali, ambazo ziliibua malalamiko mengi kutoka kwa Zanzibar.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amewataka wananchi wa Pemba, kuiunga mkono Katiba Inayopendekezwa ambayo imetoa fursa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar, kujiimarisha kiuchumi na maendeleo.
MKUTANO mkubwa wa kimataifa kuhusu masuala ya afya umeelezwa kuwa ugonjwa wa ebola umethibitisha kuwa dunia haijajenga uwezo wa kutosha wa kukabiliana na magonjwa makubwa ya mlipuko.
MKAZI wa Mwanza aliyetambulika kwa jina la Sultan Said Ramadhani (31) maarufu kama Kusharunga, amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu kutoka Ethiopia.
ALIYEKUWA Mshauri wa Rais wa Masuala ya Utalii katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Issa Ahmed Othman ambaye alifariki dunia Januari 25 akiwa katika matibabu nchini India, amezikwa juzi katika kijiji cha Kianga nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
OFISA Elimu wa Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Julius Mduma amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kiteto na kushtakiwa kwa kosa la kujipatia Sh 5.4 milioni kwa njia ya udanganyifu.
MAMLAKA ya wanyamapori nchini inatarajia kusitisha umiliki wa vitalu vya uwindaji wa kitalii nchini, ifikapo mwaka 2018, jambo litakalosaidia mamlaka hiyo kumiliki mapori yote ya akiba na kuwa na uwezo wa kubadilisha sera ya matumizi ya mapori hayo.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umeongeza muda wa mwezi mmoja kwa wanachama wake kuweza kuhakiki taarifa zao, kabla ya kuhitimisha utaratibu huo ifikapo Februari 28, mwaka huu.
WATU wawili wameuawa katika matukio tofauti, akiwemo kijana mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake.
WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amewataka wafanyakazi kushirikiana, katika kipindi cha miezi 10 iliyobakia kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, ili kurudisha heshima na hadhi ya bandari.