WAVUVI wametakiwa kuifahamu sheria ya Uvuvi ya mwaka 2010 ambayo imelenga zaidi kupambana na vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekuwa chanzo cha kuharibu mazingira ya baharini.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa, Wilaya za Kilombero na Ulanga kufanya ukaguzi wa bonde la Kilombero kuona maendeleo yake.
WAFUGAJI jamii ya Wamasai kutoka Mabwegere na Kambala wilayani Mvomero mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuunda tume huru kuchunguza tatizo la migogoro ya ardhi na kutoa suluhisho la kudumu kwa kuzingatia haki na usawa.
NAIBU Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Kaika Telele amewataka wahifadhi wa Bahari Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma kuhakikisha kuwa wanamaliza tatizo la uvuvi haramu unaotumia baruti sambamba na kuendelea na kuhifadhi mazingira ya bahari na viumbe vilivyomo.
UELEWA duni katika jamii za wafugaji, unasababisha kukwama kwa jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu, kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanza shule wanapata elimu ya msingi.
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Same wameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha za ruzuku ya serikali zaidi ya Sh milioni 2 unaodaiwa kufanywa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mbakweni, Kijiji cha Msindo wilayani humo.
WANANCHI mkoani Tabora wamelalamikia askari mgambo wa Halmashauri ya Manispaa Tabora waliopo stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani kuwa ni kero na wamekuwa wakifanya utapeli wa dhahiri.
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mussa Assad ameishauri Serikali na Bunge kuangalia upya vyanzo vya mapato vya serikali na matumizi ya fedha zinazopatikana, kwa kuwa ni dhahiri hali ya fedha si nzuri serikalini kwa sasa.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma, Saada Mwaruka amewataka madiwani na watendaji kuwa waaminifu na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo fedha zinazokusanywa kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuiletea maendeleo halmashauri.
SERIKALI imesema azma yake ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma iko pale pale, licha ya wabunge kushauri iondokane na ndoto hizo kwa kuamua shughuli zake ziendelee jijini Dar es Salaam.